March 31 2016 Mwanamitindo Mtanzania Millen Magese alikaa kwenye ON AIR WITH MILLARD AYO na kumwaga machozi akielezea mateso yanayotokana na tatizo aliloligundua kwake toka akiwa na umri wa miaka 13 na mirija yake kuziba mwaka 2007.
Kuna kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.
Baada ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na Marekani, leo hii Millen anayofuraha kuitangaza habari njema kuwa amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.
Tazama hapa chini Millen Magese akiliongelea tatizo hilo lililomsumbua toka akiwa na umri wa miaka 13.
ULIPITWA? Kutana na Mtanzania Milionea Mtarajiwa aliyeacha kazi ya Mshahara wa milioni moja na kuamua kujiajiri, bonyeza play hapa chini