on air with millardayo

Baada ya oparesheni 13 Millen Magese anapanga kuondoa kizazi, ushauri wa kwenda kwa TB Joshua je?

on

Mwanamitindo Mtanzania Millen Magese ambaye amekua akiishi na kufanya kazi Marekani amechukua likizo ya mwezi mmoja kufanya kampeni ya tatizo la kiafya ambalo limekua likimsumbua toka akiwa na umri wa miaka 13 na ikaja kugundulika akiwa na miaka 26 na mpaka sasa ameshafanyiwa Oparesheni 13 kutokana na tatizo la Endometriosis linalomkabili kwa maumivu kila anapokuwa kwenye mzunguko wake kama Mwanamke.

Moja ya matokeo ya tatizo hili Millen anasema ni kusababisha kutopata mtoto na baada ya kuhangaika sana na kulipia gharama kubwa kwenye hospitali za Marekani na Afrika kusini, sasa amepanga kuoondoa kizazi mwezi April 2016 na hatua hiyo itasaidia afya yake kuwa na afadhali zaidi kuliko kipindi kilichopita.

Anasemasitakuwa naumwa kila mwezi, sitakuwa na mzunguko… Mungu akibariki nitaondoa kizazi April, hii sio mara ya kwanza kutaka kuondoa kizazi ni mara ya tatu, mara ya pili September 2015 nilifika kabisa mpaka natakiwa kuingia kusaini ili kitolewe lakini nikasema No siko tayari, huwezi kujua Mungu ana makusudi gani… atakaponiongoza nitakwenda ila siumii tena sababu kuna uwezo wa Mwanamke mwingine kunibebea mtoto wangu na nikaokoa maisha yangu kwa sababu nina mayai

Kuhusu kwenda kuombewa kwa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua, Millen amesema ‘Sijakwenda kwa TB Joshua lakini ninachoamini hakuna mtu stong kuliko Mungu, imani yangu inaweza isiwe kwenye hayo Makanisa wanayoyatamka na mimi sio mtu wa kufata mkumbo, mimi ni Mkatoliki na nakwenda ninapotaka kwenda

Kumtazama Millen zaidi na kuelewa anayoyapitia unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini…

ULIIKOSA EXCLUSIVE YA DOGO JANJA? HUTOTAKA IKUPITE TENA… ITAZAME HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments