Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema akiwa Arusha moja ya mambo atakayosimamia ni kuhakikisha Watu wanapata haki zao bila kupindishwa pamoja na kuhakikisha Watendaji wanawajibika kwenye kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akiongea wakati wa mapokezi yake Arusha leo April 08,2024, Makonda amesema “Nisipokuwa Kiongozi wa haki sitokuwa tu siwatendei haki watu wa Arusha lakini nitakuwa pia sijitendei haki Mimi mwenyewe na uzao wangu, Wananchi wanaodhulumiwa, kunyanyaswa, kucheleweshwa na kuzungushwa kupata haki zao Mimi nimekuja kusimama kwa niaba yao, kwahiyo kama kuna Mtu yupo Monduli, Ngaramtoni, Arumeru n.k ilimradi una haki yako na unajua ni haki yako, Mimi sitojali kama haujasoma, sitojali kama una pesa au una Ndugu mwenye Mamlaka nitasimama kuhakikisha haki inapatikana, Rais wa Nchi yetu ni Mtu anayetaka haki”
“Jambo la pili ni uwajibikaji, mmenipokea vizuri sana, mmenifurahia vizuri sana ila tutageukana muda sio mrefu, sitojali wewe ni nani?, Baba yako ni nani?, ulipataje hicho cheo aidha ulipata kwa kuhonga, kwa rushwa au kwa uganga nitakula sahani moja na wewe, lazima kila Mtu awajibike kwenye nafasi yake, kama ni DC, DED au Mkuu wa Idara ishike nafasi yako kisawasawa, kwenye Idara yako sijui mambo yalikuwaje , Kaka yangu Mongella anatumiaga akili sana kuwaeleza Watu Mimi huo muda sina, niwaombe Watumishi wote nataka kila Mtu ajue wajibu wake na asimame barabara kufanya kazi yake kwakuwa mshahara unaokula ni kodi za Wananchi wa kawaida wanataka wahudumiwe kisawasawa”