Habari za Mastaa

VIDEO: Hasira za Nicki Minaj baada ya kuona mlinzi wake anachezea simu badala ya kumlinda

on

Hii ishu imetokea wakati Nicki Minaj akifanya show Dubai na kilichotokea ni kwamba Mlinzi wake huyo hakuwa makini na kazi, wakati Nicki yuko kwenye stage anaimba, akagundua kwamba upande wake wa kulia mmoja wa Walinzi wake hafanyi kazi inavyotakiwa maana kashika simu yake ya mkononi.

Nicki alichofanya ni kwenda kumnyang’anya ile simu alafu akaitupa nyuma ya stage kwenye upande ambao watu wake wengine walikuwepo na haikujulikana kama Nicki Minaj aliongea chochote baada ya show kumalizika ila media zimeripoti kukasirika kwake na kushindwa kujizuia kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini.

.

Kitendo cha Nicki kutupa hiyo simu kimepokelewa tofauti, kuna wengine wamesema ni sawa sababu amemlipa yule jamaa kwa ajili ya kumlinda na sio kushika simu wakati wa kazi, wengine wamesema Nicki ameonyesha ni kiasi gani hana adabu kwa sababu angeweza kuvumilia hiyo ikapita.

nicki 2 nicki 1

ULIIKOSA YA WATOTO WA KITANZANIA KUJITOKEZA BAADA YA KUSIKIA VANESSA MDEE ANATAFUTA DANCERS? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments