Habari za Mastaa

Nicki Minaj na Meek Mill ni wapenzi… je mama yake Nicki anauonaje uhusiano wao?

on

Nicki Minaj ametoka kumaliza tour yake ya The Pinkprint Tour Marekani siku chache zilizopita na kote huko alikuwa anatembea na mpenzi wake Meek Mill… Siku chache zilizopita Nicki na Meek Mill walifanya interview na gazeti kubwa la mitindo Marekani na miongoni mwa vitu ambavyo Nicki Minaj aligusia ni uhusiano wake na rapper Meek Mill.

mmmmm2

Nicki Minaj & Meek Mill.

Je unajua kuwa mpaka leo mama yake Nicki Minaj hataki Nicki na Meek Mill wawe pamoja?… na kumbe katika maisha yake yote Nicki Minaj amewahi kuwa wanaume 3 tu kimapenzi!… akiwa kwenye interview hiyo Nicki alisema..

>>> “mama yangu anamjua Meek Mill kwa kile anachokiona kwenye media na mitandao ya kijamii… na siku zote huwa anajaribu kuhakikisha kama kweli Meek Mill ana nia njema na mimi (mama bwana)… kingine ambacho huwa kinamfanya mama yangu awe hivyo ni kwasababu mimi maisha yangu yote nimekuwa na wapenzi 3 tu…<<< Nicki Minaj.

mmmm

>>> “Sijawahi kutembea ovyo… sina utalaamu sana kwenye hayo mambo, kila mtu alihofia kuwa nitaumizwa… hata mchungaji wangu alihofia uhusiano wangu na Meek.. mama yangu ndio kabisa mpaka leo hana amani na wala hajamkubali Meek Mill kwasababu anajua kuwa mimi nikipenda napenda na kila kitu nilichonacho na haamini kama Meek Mill ataniheshimu na kuthamini upendo wangu, na wala haamini kuwa Meek ananifaa (my mother is overprotective), na kila siku anahakikisha najua hilo na ananisihi niwe mwangalifu!” <<< Nicki Minaj.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments