Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Miradi 630 ya Dola Bilioni 3.68 imesajiliwa
Share
Notification Show More
Latest News
Sudan:Burhan aonya vita vya Sudan vinaweza kusambaa hadi kwa majirani
September 22, 2023
Tunisia yamwachilia mchora katuni aliye kamatwa kwa michoro inayomdhihaki waziri mkuu
September 22, 2023
Wanafunzi 90 wa shule ya msingi wamelazwa hospitalini baada ya kula keki zenye bangi
September 22, 2023
Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 22, 2023
September 22, 2023
NEMC yatoa siku saba kwa Uongozi wa kiwanda kichotengeneza Wadudu, harufu kali yalalamikiwa
September 22, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Miradi 630 ya Dola Bilioni 3.68 imesajiliwa
Top Stories

Miradi 630 ya Dola Bilioni 3.68 imesajiliwa

January 19, 2023
Share
4 Min Read
SHARE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 miradi mipya ya uwekezaji 630 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.68 inayotekelezwa na makampuni ya India imesajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Amesema hatua hiyo inatokana na jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine kutoka nchini India waje wawekeze Tanzania.

Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokutana na ujumbe wa Bunge la India (Lock Sabha) ulioongozwa na Spika wa Bunge hilo, Mheshimiwa OM Birla. Waziri Mkuu kutana na viongozi hao kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ambaye yupo nje ya nchi kikazi.

Majaliwa amesema Nchi ya India na Tanzania zimekuwa na ushirikiano Mkubwa wa kiuchumi na biashara huku India ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na ushirikiano wa biashara unaofikia Dola za Marekani bilioni 4.58 kwa mwaka 2021 – 2022.

Waziri Mkuu amemuhakikishia Spika huyo kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati yake na India. “Rais anamatumaini makubwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi ya Tanzania na India na kwamba ushirikiano huo umekuwa na manufaa makubwa kati ya nchi zetu.”

Amesema Tanzania na India zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, nishati, maji, elimu, afya, biashara na teknolojia na hivyo kuleta manufaa makubwa.“Rais amefurahia ujio wako Nchini Tanzania, ni matarajio yake kuwa ujio huu utakuwa na manafuu makubwa baina ya Nchi zetu.”

“Mwezi juni 2022 tumeshuhudia makampuni sita kutoka nchini India yakitia saini mikataba ya miradi ya maji kwa miji 28 yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 500 ambayo ikikamilika itawawezesha watanzania zaidi ya milioni sita kupata maji ya uhakika.”

“Nitoe wito kwa Nchi ya India ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa Nchi za G 20, kuwa mtetezi wa Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania katika suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa, Usalama wa chakula, uwezeshaji wa wanawake na vijana pamoja na kupambana na athari za uviko 19”

Kadhalika, Majaliwa amesema ujio wa Spika huyo na ujumbe alioongozana nao utaboresha uhusiano baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la India kwa wabunge na viongozi wa mabunge hayo kubadilishana uzoefu.“Nitoe wito kwa mabunge yetu haya kuweka utaratibu wa kutembeleana na kubadirishana uzoefu, ili kukuza ushirikiano.”

Pia, Majaliwa ameishukuru Serikali ya India kwa ushirikiano na namna ambavyo imeendela kutoa fursa za masomo kwa wataalam wa Tanzania katika sekta mbalimbali nakuiomba nchi hiyo iendelee kutoa ufadhili huo wa masomo katika nyanja nyingine za teknolojia ya mawasiliano, afya, uhandisi, kilimo, maji, madini na gesi.

Kwa Upande wake, Spika wa Bunge la India Mheshimiwa Birla amesema, Bunge la India litakuwa msemaji mzuri wa ushirikiano na maendeleo baina ya Tanzania na India ili nchi hizo ziendelee kunufaika na ushirikiano uliopo.

“Kwa niaba ya Serikali na Bunge la India, tunawasilisha pongezi zetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake wa mfano, sasa tunaona uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi na tunaona miradi mikubwa ikitekelezwa, tafadhali fikisha pongezi zetu kwake.”

Birla na ujumbe wake yuko katika ziara ya kikazi ya siku tatu Nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea vituo mbalimbali vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama.

You Might Also Like

Sudan:Burhan aonya vita vya Sudan vinaweza kusambaa hadi kwa majirani

Tunisia yamwachilia mchora katuni aliye kamatwa kwa michoro inayomdhihaki waziri mkuu

Wanafunzi 90 wa shule ya msingi wamelazwa hospitalini baada ya kula keki zenye bangi

NEMC yatoa siku saba kwa Uongozi wa kiwanda kichotengeneza Wadudu, harufu kali yalalamikiwa

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 22, 2023

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA January 19, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Huduma ya kujipima UKIMWI mahala pa kazi
Next Article Wadau sekta ya usafirishaji kukutanishwa pamoja, “Tutajadili changamoto mbele ya Waziri Mbarawa”
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Sudan:Burhan aonya vita vya Sudan vinaweza kusambaa hadi kwa majirani
Top Stories September 22, 2023
Tunisia yamwachilia mchora katuni aliye kamatwa kwa michoro inayomdhihaki waziri mkuu
Top Stories September 22, 2023
Wanafunzi 90 wa shule ya msingi wamelazwa hospitalini baada ya kula keki zenye bangi
Top Stories September 22, 2023
Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 22, 2023
Magazeti September 22, 2023

You Might also Like

Magazeti

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 21, 2023

September 21, 2023
Magazeti

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 19, 2023

September 19, 2023
Magazeti

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 19, 2023

September 19, 2023
Magazeti

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 18, 2023

September 18, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?