Mwanamitindo Mnigeria Victoria Chiamaka ameshiriki kwenye mashindano ya Miss Africa huko Russia akiwa na bendera ya Nigeria yenye rangi ya damu katikati akiwa na nia ya kupinga mauaji ya Vijana waliouwawa na Majeshi ya Nigeria wakati wakifanya maandamano ya End Sars Nchini humo October 2020.
Mwanamitindo huyu ambaye pia ni Mwanafunzi hakushinda kwenye shindano hili lakini alikua miongoni mwa Warembo wachache waliokubalika na Mashabiki.
Udeh (23) aliiambia CNN kwamba hakujali Majaji wa Shindano hilo watawaza nini kuhusu alichokifanya bali alichojali kwa wakati huo kilikua ni kufikisha ujumbe wake akisema alama nyekundu ya damu kwenye bendera hiyo iliashiria damu za Vijana zilizomwagika kwenye maandamano hayo.
GONDWE ASHTUKIZA SOKONI MAGOMENI, ATOA MAAGIZO “WALIOKO NJE WAINGIE NDANI KUFANYA BIASHARA”