Habari za Mastaa

Shindano jipya limeletwa linaitwa Miss Kilimanjaro! halihusiani na jingine lolote la Umiss.

on

.

.

Shindano la kumsaka mrembo atakayeuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye shughuli mbalimbali za kijamii limezinduliwa June 24 2015 ambapo litakuwa na washiriki 20 watakaowania taji hilo July 24 2015 Kili Home Resort.

Mkurugenzi Jacqueline Chuwa amesema ‘sisi kama waandaji wa kumtafuta mwakilishi au balozi Miss Kilimanjaro, nia ya kumtafuta Miss Kilimanjaro au mwakilishi wa mkoa wa kilimanjaro kwanza ni kutangaza vivutio ambavyo vipo kwenye mkoa wa kilimanjaro kama Chemchem ya maji ya moto kule boma, Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine’

‘Mimi kama Miss Kilimanjaro niliyepitia huko nyuma nimeona ngoja niandae tamasha hili la kumsaka mrembo wa Miss Kilimanjaro, tamasha hili limesajiliwa maalumu kwa mkoa wa Kilimanjaro na halihusiani na mashindano ya umiss ya aina yoyote…’

Msikilize hapa

.

.

Hawa ni baadhi ya warembo watakaowania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 kwenye ukumbi wa Kill Home Resort mkoani Kilimanjaro.

.

.

.

.

3X6A9877[1]

.

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments