Habari za Mastaa

Hii ndio kamati mpya itakayosimamia shindano la Miss Tanzania akiwemo na Jokate Mwegelo

on

.

.

Najua nina watu wangu wanaopenda headline za Ma Miss sasa good news ninayotaka kukupatia ni kwamba shindano la kumsaka mrembo Miss Tanzania limerudi rasmi, na leo kulifanyika utambulisho wa kamati mpya itakayohusika kusimamia tamasha hilo.

Kwa mujibu wa msemaji wa kamati hiyo mpya, Jokate Mwegelo..‘Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu ns kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

.

Picha ni wajumbe wa kamati mpya ya Miss Tanzania, Jokate na Juma Pinto (Katikati Mwenyekiti wa kamati hiyo).

‘Tumekubali na tumepokea majukumu hayo na kuahidi kusimamia kanuni, Sheria na Taratibu za kuendesha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.Tunaomba jamii ya Watanzania watupe ushirikiano pamoja na kutuamini kwamba tunaweza kuisogeza mbele zaidi tasnia hii ya urembo hapa nchini’ – Jokate Mwegelo

Kwa leo hatutakuwa na mengi ya kusema kwa sababu ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili hivyo kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka yetu  ya Tanzania’ – Jokate Mwegelo

3X6A5818

Wajumbe wa kamati mpya ya Miss Tanzania, Jokate Mwegelo na Juma Pinto ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.

3X6A5832

Waandishi wa Habari.

.

Miss Tanzania 2014, Lilian Kamazima.

Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao

1.Juma Pinto – Mwenyekiti

2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti

3.Doris Mollel – Katibu Mkuu

4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati

5.Hoyce Temu – Mjumbe

6.Mohamed Bawazir – Mjumbe

7.Gladyz Shao – Mjumbe

8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe

9.Shah Ramadhani – Mjumbe

10.Hamm Hashim – Mjumbe

11Khalfani Saleh – Mjumbe

12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni

1.Dr.Ramesh Shah

2.Hidan Ricco

3.Yasson Mashaka

4.Deo Kapteni

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments