Habari za Mastaa

Missy Elliott arudi kwa kishindo baada ya ukimya wa miaka 10 na WTF (Where They From) – (Video)!

on

Mara ya mwisho kumsikia Missy Elliott kwenye headlines za burudani ilikuwa ni lini? Amini usiamini imepita miaka 10 toka mkongwe wa muziki wa HipHop Missy Elliott aziweke headlines kwenye kurasa za muziki duniani na kama wewe ni miongoni wa mashabiki wakubwa wa Missy Elliott basi ipokee hii good news popote pale ulipo.

Missy Elliott amerudi na single yake ya kwanza ndani ya miaka 10, wimbo unaitwa WTF (Where They From) na ndani mkali wa hit single ya Happy, Pharrell Williams ameshirikishwa.

missy

Missy Elliott & Pharrell Williams.

Licha ya Missy kufanya kazi na Pharrell, msanii huyo wa muziki wa HipHop amekuwa studio kwa miezi kadhaa sasa akikamilisha Album yake ya kwanza ndani ya miaka 10 na Rapper, Producer Timbaland ambaye pia mikono yake ilihusika kwenye Album ya Missy Elliott, Cookbook ya mwaka 2005.

Welcome back Missy Elliott!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments