Mitambo mipya itakayo harakisha upakiaji na ushushwaji wa shehena ya makasha ya mizigo imewasili katika Bandari ya DSM na tayari wataalamu wameshaanza kuifunga ili ifikapo mwishoni mwa mwezi January mwakani ianze kufanya kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema ujio wa mitambo hiyo utaongeza ufanisi bandarini kwani awali mitambo ya zamani iliweza kushusha makasha kati ya 15 hadi 18 kwa saa moja, lakini mtambo mpya ukikamilika kufungwa utaweza kupakua makasha kati ya 35 hadi 38 kwa saa.