Habari za Mastaa

Stori za Facebook, Twitter, Instagram, Blogs leo January 27, 2015 ziko hapa

on

.

.

Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.


Facebook:

Mwanachi: MAANDAMANO: Prof. Lipumba,wafuasi 32 wa CUF wakamatwa na polisi
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.
Awali polisi ilizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.

Blog

Michuzi: TRILIONI MOJA KUTUMIKA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM.
SERIKALI imedhamiria kupunguza msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam kwakujenga barabara sita zitakazo ambazo ujenzi wake utasimamiwa na TANROADS. Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. trilioni moja ambapo lengo barabara hizo ni kupunguza adha ya msongamano wa magari katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es saalam.

Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara hizo. “Barabara hizi zinajenga kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na lengo kubwa la mradi huu ni kupunguza msongamano ndani ya jiji” alisema Magufuli.

Magufuli aliendelea kusema “Rai yangu kwa Watanzania wote ikiwemo madereva wa magari yenye uzito mkubwa kuacha kupita barabara zisizo stahimili uzito wa magari hayo na kuwaasa wananchi wa maeneo jirani waache kugeuza barabara hizo kuwa maduka au fremu za biashara”.

Mtanzania
Katika gazeti letu la Mtanzania toleo No. 7709 la Alhamisi Januari 22, mwaka huu, tuliandika kimakosa stori yenye kichwa cha habari ‘Wema Sepetu ampeleka Diamond Polisi’. Baada ya kufanya uchunguzi tumejiridhisha habari ile haikuwa na ukweli, kwani chanzo kilichotupatia kilitupotosha, hivyo kuleta usumbufu kwa msanii Wema pamoja na jamii. Kutokana na hali hiyo, tunapenda kumwomba radhi Wema na familia yake. Siku zote sisi MTANZANIA tumekuwa makini katika kusimamia misingi ya habari za weledi na haki kwa jamii.

BBC: Wanajeshi wawaua waasi waliojisalimisha
Wakazi wa kazkazini magharibi mwa Burundi wameiambia BBC kwamba walishuhudia wanajeshi wa serikali wakiwaua waasi waliojisalimisha.Wanakijiji wa mkoa wa Cibitoke walisema kuwa takriban waasi 17 walipigwa risasi na kuuawa mapema mwezi huu baada ya kusalimu silaha zao.

Hivisasa.co.tz
Watu wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha Kibambila wilayani Kakonko mkoa wa Kigoma wamefariki dunia huku mmoja akinusurikia kutokana na kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mganga wa zamu katika kituo cha Afya cha Kakonko, Ndalikunda Kweka, alisema kuwa watu hao wanne walifikishwa kituoni wakiwa na hali mbaya na kwamba kwa bahati mbaya walifariki dunia wakati wahudumu wa afya wakijitahidi kuokoa maisha yao.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Kakonko, Fadhili Seleman aliwataja watu waliokufa kuwa ni pamoja na Neema Joseph (12), Jonas Joseph (18) Yusuph Joseph na Majaliwa Joseph (11). Selemani alisema kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na wahudumu wa afya kituoni hapo na baada ya kumhoji mtu aliyenusurika kwenye tukio hilo unaonyesha kuwa watu hao walikula ugali unaosadikiwa kuwa ulikuwa na sumu.

Majimbo saba yatangaza hali ya Hatari
Hali ya tahadhari imetangazwa katika majimbo saba ya Marekani, wakati wa kukabiliwa na upepo mkali mithili ya Kimbunga huku kukiwa na theluji yenye upana wa SM 90 kaskazini-Mashariki.

Saleh Jembe:

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema atajua zaidi kuhusiana na hali yake hapo baadaye.
Okwi amesema atajua kuhusiana na hali yake angalau baada ya kuanza mazoezi.
“Najisikia vizuri kwa sasa. Ila nikianza mazoezi nitajua vizuri zaidi,” alisema Okwi.

Okwi alianguka na kuzimia baada ya kugongwa na beki Aggrey Morris wa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda anatarajia kuanza mazoezi leo akiwa na kikosi chake cha Simba.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments