fB insta twitter

Stori za Facebook,Twitter, Instagram, Blogs February 18, 2015 ziko hapa

on

.

.

Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.

Michuzi:
Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Rashidi Makwaro aka Chid Benz leo amekiri mahakamani mashitaka matatu yanayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya shilingi. 38,638 , bangi ya sh 1720 na vifaa vya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz alikiri mashitaka hayo baada ya kusomewa upya hati yake ya mashitaka mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Warialwande Lema.
Hakimu Lema alisema kuwa mshtakiwa amekiri mashitaka yake mahakamani itasikilizwa maelezo ya awali February 23, mwaka huu.

Hivi sasa.co.tz
Mwili wa Mtoto Mwenye ualbino wapatikana msituni
Mwili wa mtoto wa mwaka mmoja mwenye ulemavu wa ngozi Yohana Bahati aliyeporwa mikononi mwa mama yake juzi Mkoani Geita, umeonekana jana jioni ukiwa umekatwa miguu na mikono yote na kufukiwa ardhini kwenye hifadhi ya msitu wa Biharamulo, Wilayani Chato.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema mwili wa mtoto huyo umebainika jana majira ya saa 12:30 jioni ukiwa umefukiwa kwenye eneo ambalo linashamba la mahindi.
Mtoto mwingine mwenye ulemavu wa ngozi aliyeporwa mwezi desemba mwaka jana bado hajapatikana hadi leo licha ya jeshi la Polisi kungatangaza kutoa zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazo saidia kupatikana mtoto huyo.
Mauaji, ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi bado ni changamoto licha ya serikali kutafuta mbinu za aina mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuwapiga marufuku wapiga ramli.

BBC
Wayne Rooney aomba radhi
Golikipa wa timu ya Preston Thorsten Stuckmann ameeleza kuwa mshambuliaji Wayne Rooney
alimuomba msamaha baada ya kuanguka katika eneo la hatari na kupata mkwaju wa penati.
Kipa huyu alimwangusha Rooney wakati mchezaji huyo akielekea kufunga bao na kusababisha penati,
Stuckmann, alisema “Rooney aliniomba msamahani na kuniambia ilikua ni nafasi yake ya kupata penati”.
“Naamini tukio kama lile lingetokea kwenye goli la Manchester United toka kwa mshambuliaji wetu refa asingeweza kutupa penati sina shaka na hilo”.
“Sisemi kama haikuwa penati, nachokisema hakukua na mgongano wowote”
Rooney alifunga mkwaju huo wa penati na kuipa timu yake ushindi mnono wa mabo 3-1dhidi ya Preston.

Ubaguzi wa mashabiki wa Chelsea watolewa

Kanda ya video inayowaonyesha mashabiki wa kilabu ya Chelsea wakimzuia mtu mweusi kuingia katika treni mjini Paris imetolewa.

Katika kanda hiyo mtu huyo anaonekana kujaribu kuingia katika treni hiyo lakini anasukumwa nje.
Kundi moja la watu baadaye linasikika likiimba: ”we are racist,racist and that’s how we like it” {sisi ni wabaguzi,wabaguzi na hivyo ndivyo tupendavyo}.
Tukio hilo lilifanyika kabla ya mechi ya kilabu bingwa katika mji wa Paris.
Kilabu ya Chelsea imesema itawasaidia maafisa wa polisi na mashabiki wowote waliohusika watakabiliwa na marufuku.
Kanda hiyo ya video illitolewa na Guardian,ambalo liliripoti kisa hicho kufanyika katika kituo cha Richelieu-Drout katikati ya mji wa Paris siku ya jumanne jioni.
Sauti nyengine ilisikika ikiimba: ”Chelsea,Chelsea,Chelsea”
Rweyunga
MALAWI KUTUNGA SHERIA YA KUDHIBITI NDOA ZA UTOTONI
Nchi ya Malawi inatarajia kuridhia sheria mpya inayopiga marufuku ndoa za watoto ambapo taifa hilo kwa sasa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ndoa za watoto duniani.
Wabunge wa nchi hiyo ndogo ya kusini mwa Afrika wiki iliyopita walipitisha muswada ambao unataongeza umri wa kuoa kutoka umri wa miaka 16 hadi miaka 18.
Wanaharakati za haki za binadamu na wabunge wanasema Malawi inandoa nyingi za watoto, ambapo watoto wa kike wenye umri wa miaka 10 huozwa.
Chini ya Sheria za nchi hiyo rais Peter Mutharika anamuda wa wiki tatu za kutia saini muswada huo wa ndoa, talaka na mahusiano ya familia ili kuwa sheria baada ya kuidhinishwa na wabunge kesho.
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA SHAMARIWA A KATA YA IGOMA AKUTWA AKIWA KAJINYONGA
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Shamariwa A kata ya Igoma wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Julias Makoye (CCM), amekutwa amejinyonga juu ya mti ulio jirani na nyumba yake usiku wa kuamkia leo.
Makoye alishinda kiti hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana, akiwa ameongoza mtaa huo kwa awamu ya pili baada ya kuongoza miaka mitano iliyopita.
Mke wa marehemu, Ivona Polikalapo, amesema jana saa 10 jioni alimsikia mumewe akiongea na mtu kwenye simu yake ya mkononi na kumsisitiza anahitaji mzigo wake wote.
Amesema ilipofika saa 10 alfajiri leo, mbwa wao walisikika wakibweka kwa muda mrefu hali iliyomfanya marehemu atoke nje kuangalia kilichopo katika banda lao la mifugo huku (mke) akiendelea kuandaa chakula cha mifugo.
Mama huyo anasema baada ya muda alitoka nje kwenda kumwaga uchafu shimoni, lakini alishangazwa kumuona ananing’inia juu ya mti na alipojaribu kumuita hakuweza kuitika.

Hata hivyo, kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Japhet Lusingu, amethibitisha kuwapo na tukio hilo na kusema amejinyonga huku chanzo chake hakijafahamika.
Katavu Blog
WANAKIJIJI WAVAMIA KAMBI YA KAMPUNI YA UCHIMBAJI WA MADINI WACHOMA GARI MOTO
Wananchi wa Kijiji cha Ibindi Kata ya Machimboni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamevamia kambi ya Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Sambulu Mining na kuchoma moto gari la Kampuni hiyo na vitu mbalimbali baada ya watumishi wa Kampuni hiyo kumkamata mwanajijiji mwenzao na kisha kumkata na panga kwa kumtuhumu kuiba mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya Dhahabu yenye kilo mbili ya thamani ya milioni 90.
Bongo Movies
Bodi Ya Filamu Yazuia Filamu ya “Fifty Shades of Grey
Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976.

Saleh Jembe
Kiungo wa zamani wa Simba, Mrundi, Pierre Kwizera, amebamba dili baada ya kufanikiwa kujiunga na timu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda.
Kiungo huyo ambaye aliichezea Simba kabla ya kufungashiwa virago sambamba na ‘ndugu yake’, Amissi Tambwe, amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu, lakini kama uwezo wake ‘utawakuna’ mabosi wake, ataongezewa mkataba.
Akizungumza kutoka jijini Kigali, Rwanda, kiungo huyo alisema kuwa anafurahia maisha mapya ndani ya klabu hiyo inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Ninamshukuru Mungu nimepata timu, nipo na Rayon Sports ya Kigali. Wamenipokea vizuri na ninafurahi kuwa hapa, wikiendi walikuwa Cameroon kucheza mashindano ya Caf.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments