Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Tarehe 30 January PAC inakutana na Shirika la TPDC hapa dodoma kuhusu mahesabu ya Shirika na uwazi wa mikataba ya Gesi Asilia na Mafuta
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) January 28, 2015
Facebook:
Zitto:Kwanini sikwenda kusoma taarifa ya PAC leo nilipoitwa na Spika? Jibu rahisi kabisa, siwezi kuona madhila na uvunjifu mkubwa wa HAKI za binaadamu nikaendelea na mambo kama hakuna lililotokea. Kitendo cha polisi kutumia nguvu, kupiga raia hovyo na kumdhalilisha Kiongozi wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote.
CloudsFM: MICHEZO LUIS FIGO AJITOSA KUWANIA URAIS WA FIFA
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametoa taarifa za kushitusha baada ya kutangaza kuwania Uraisi wa FIFA.
Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Sporting Lisbon, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan mwenye miaka 42 anaungana na mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola katika kuwania nafasi ya kumng’oa madarakani bosi wa sasa Sepp Blatter katika chombo hicho kikubwa cha soka duniani.
Wengine wanaowania kiti hicho mpaka sasa ni Mfalme Ali wa Jordan, Michael van Praag na Jerome Champagne.
Blatter amekuwa kiongozi wa shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na akitaka kuendelea kuwania tena uongozi katika awamu ya tano.
Wagombea wote wanaowania kiti hicho wanatakiwa kujiandikisha kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Alhamisi.
Blog
BBC: England yakufuru usajili wa wachezaji
England ndiyo iliyotumia kiasi cha juu kabisa duniani, kwa timu zake kulipa dola bilioni moja nukta mbili mwaka 2014.
Vilabu vya Hispania vilishika nafasi ya pili kwa matumizi ya uhamisho wa wachezaji, vikitumia dola milioni mia saba.
Takwimu hizo pia zinabainisha kuwa India ilisajili wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wote duniani kwa wastani, na China ikiingia katika kundi la nchi kumi za kwanza katika matumizi ya uhamisho kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Takwimu hizi mpya hazihusishi uhamisho wa wachezaji kati ya timu moja na nyingine ndani ya nchi husika.
Hivisasa.co.tz:
Kagera, kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa katika vichaka eneo karibu na kambi ya Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia kata ya Nshambya.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, Kaimu Mtendaji wa kata ya Nshambya, Christian Ngaiza, alisema alipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa dereva wa bodaboda kuwa kuna mtu ameuawa lakini wananchi wanaogopa kutoa taarifa Polisi.
Mwili huo uligundulika majira ya saa sita mchana baada ya watu waliopita katika eneo hilo kuuona ukiwa umelazwa karibu na moja ya shamba lililopo mtaa wa Bunkango eneo la kambi hiyo ya Polisi. Mwili huo ulikuwa na majeraha maeneo ya usoni kiasi cha kushindwa kutambulika kirahisi.
Kwa mujibu wa kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ambaye pia ni mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo, Gilles Mroto alisema ametuma timu ya maofisa wa Polisi kwenda eneo la tukio kufanya uchunguzi
Mwili huo haukuweza kutambulika na hivyo kuzikwa na Manispaa ya Bukoba katika makaburi ya Kyebitembe.
Rweyunga.blogspot.com
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanya biashara apandishwa kizimbani
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja amefikishwa mahakamani ya wilaya ya Dodoma akikabiliwa na mashtaka mawili ya kwachochea wafanya biashara wa mkoa wa Dodoma kutenda kosa na kuwazuia wafanya biashara hao kulipa kodi kwa kutumia mashine za kieletroniki za Efds.
Full Shangwe.blog:JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 21 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI.
Katika msako wa kwanza, jeshi la polisi mkoa wa mbeya linamshikilia ndaizaba selepin (25) na wenzake kumi na tano [15], kati yao watu wazima 08 na watoto 08, wote ni raia na wakazi wa nchini burundi wakiwa wameingia nchini bila kibali.
Wahamiaji hao walikamatwa mnamo tarehe 27.01.2015 majira ya saa 04:00 usiku huko katika kijiji cha kandete, kata ya itope, tarafa ya unyakyusa, wilaya ya kyela, mkoa wa mbeya.
Father Kidevu:Lipumba afikishwa mahakama hakimu mkazi kisutu
Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF, Prof Ibrahim haruna Lipumba afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kujibu shitaka la kuhamasisha wanachama wa chama chake kufanya jinai.
Saleh Jembe: KIEMBA TAYARI KUANZA MAZUNGUMZO, AWAKARIBISHA YANGA
Kiungo mkongwe wa Simba anayeichezea Azam FC kwa mkopo, Amri Kiemba, amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kuanza mazungumzo na timu yoyote inayomhitaji hata ikiwa Yanga.
Kiemba yupo Azam kwa mkopo na mpaka msimu huu utakapomalizika, atakuwa amebakiza miezi sita.
Kiemba amefunguka kuwa, soka ndiyo kazi yake, hivyo anaweza kutua timu yoyote kama ataelewana nao hata kama ikiwa Yanga ambao ni mahasimu wa Simba, yupo tayari kwenda kuitumikia.
“Sijajua nitakwenda wapi baada ya kumalizana na Simba na nikishatoka kwa mkopo hapa Azam mwisho wa msimu, timu yoyote naweza kuzungumza nayo kuanzia sasa kwa ajili ya kujua msimu ukiisha nakwenda wapi.
“Mpira ni kazi yangu, kwa hiyo siwezi kuchagua timu kwa kuwa mpira ni uleule, cha msingi ni juhudi, hata kama Yanga watakuja nitazungumza nao, kama tutakaa chini na kuelewana hakutakuwa na tatizo,” alisema Kiemba.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook