Mchungaji Peter Mitimingi wa Kanisa la Ghala la Chakula cha Uzima (Warehouse Christian Centre-WCC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Voice of Hope Ministry (VHM) inayojihusisha na huduma ya injili vijijini amefariki Dunia akiwa Muhimbili kwenye matibabu, Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo amethibitisha na kuelekezea chanzo cha kifo chake.
“Yeye alikuwa anaumwa Sukari ilipanda, ikaanza homa ya mapafu kwasababu alikuwa Arusha akapigwa na mvua kukawa na baridi kali hiyo hali ikamsumbua na kupelekea kufariki “-Mchungaji Samweli, Msaidizi wa Kanisa