Licha ya Bandari ya Mkoa wa Kigoma kuhudumia shehena za mizigo tani laki moja na elfu tisini na sita na kusababisha kupanda kwa mapato na kufikia Bilioni 6.8 kwa kipindi cha mwaka 2017/ 18 bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa shehena za mafuta.
Hayo yamebainika mara baada ya Mkuu wa Mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kutembelea bandari hiyo kwa lengo la kuangalia miundombinu ya usafirishaji ya bandari na reli lakini pia kuzunagumza na wadau wa usafirishaji.
Akizungumzia suala la kufungwa kwa shughuli za bandari ifikapo saa 12 jioni kutokana na sababu za kiusalama RC Kigoma Maganga amesema tathimin za kitaalamu zitafanyika ili kufikia muafaka wa pamoja.
Dakika 4 za Mbowe mbele ya Lowassa “tushindane kwa hoja, usitake nikusikilize wewe tu”