January 4, 2019 Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani nchini Dkt. Charles Msonde ametoa taarifa ya matokeo mitihani ya upimaji wa Kitaifa wa Darasa la nne na Kidato cha pili ambapo ameelezea tukio la Wanafunzi tisa wa Kidato cha pili wanaodaiwa kuandika matusi katika karatasi zao za mitihani na maamuzi ambayo Serikali imeyachukua kwa wahusika.
“Baraza la mitihani Tanzania limeyafuta matokeo yote ya watahiniwa tisa wa kidato cha pili walioandika matusi kwenye script zao katika na tumeelekeza bodi za shule kuwachukulia hatua za kinidhamu ili kukomesha tabia hii ya wanafunzi”-Dkt. Charles Msonde Katibu mtendaji baraza la mitihani Tanzania.
IKULU LEO JPM “TUMBUENI HAO MCHWA WENGINE NILETEENI HATA LEO”