Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Zuwena Mohammed maarufu kama ‘Shilole’ akitumbuiza pamoja na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani (IWD) ambapo kampuni hiyo imeadhimisha kwa kutambua umuhimu wa mwanamke katika maendeleao ya jamii na taaisi.
……..
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) jana waliungana kwa pamoja kuadhimisha siku hiyo huku wakihimizwa kujiamini sehemu za kazi.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie,Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi pamoja na wafanyakazi kutoka idara mbalimbali.
Mbali na Dar es Salaam maadhimisho hayo yalifanyika katika viwanda vilivyopo Mwanza na Moshi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kampuni hiyo imekuwa ikiweka mkazo katika kuwainua wanawake katika nafasi mbalimbali ili kufikia usawa wa kijinsia kwakuwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamiii na taasisi.
Usawa wa kijinsia umehimizwa katika maadhimisho yam waka huu kupitia kauli mbiu isemayo “Badili Fikra kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”.
“Wanawake wamekuwa msingi mkubwa katika nyanja za ufanyaji maamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi maeneo ya kazi hivyo kuna haja ya kutoa nafasi kwa wanawake wengi zaidi kwenye taasisi zetu ili kufikia usawa wa kijinsia na zaidi kufikia maendeeleo endelevu,” alisema Weesie.
Hatahivyo, aliwataka wanawake kujiamini zaidi ili waweze kupata nafasi za juu huku akihimiza kutosita kuonyesha ujuzi walionao kwani ndiyo msingi wa mafanikio.
Naye, Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) Mary Rusimbi alisema wanawake wameendelea kushiriki kwa kasi katika ngazi za uongozi katika jamii na taasisi na kwamba hiyo ni ishara nzuri katika kuufikia usawa wa kijinsia hapa nchini.
Aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake na kuwapa jukwaa maalumu la wanawake liitwalo ‘SBL Spirited women’ ili kutoa nafasi ya kuboresha utendaji wao.
“Wanawake ni viongozi sio tu katika kuongeza tija lakini ni viongozi katika kushika shirika likae pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi wanazozifanya endapo ujuzi wao utatumika vizuri,” alisema Rusimbi.