Halima Idd mjane mwenye umri wa miaka 55 mkazi wa kata ya Magomeni Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amefanikiwa kujenga nyumba ya kisasa baada ya kufanya biashara ya kuuza maziwa Kwa miaka 10
Halima anasema mwaka 2015 Serikali kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) alipokea fedha ambazo alizigawanya katika makundi mawili kusomesha watoto wake pamoja na kuanzisha biashara ya kuuza maziwa .
Anasema baada ya muda wa miaka mwili alianza kufunga kuku huku biashara ya maziwa ikifanikiwa zaidi na kusafirisha hadi mkoani Dodoma ambapo alianza na mtaji wa lita 20 na kufika lita 200.
Anasema baada ya kuendelea kwa shughuli zake alianza kulima shamba hekari 3 na badaye kununua tofali na kujenga nyumba ya kisasa ambapo awali alikua akiishi nyumba ya Udongo.
Halima ameishukuru Serikali kwa kumwezesha ambapo ombi lake mradi huu kuendelea kuwezeshwa watu wengine pamoja na kutoa elimu namna ya kufanya kazi mbalimbali zinazoweza kuwaingiza kipato.
Licha ya kufanikiwa kujenga nyumba ya kisasa ya vyumba 3 pia ameweza kusomesha watoto wake wawili hadi elimu ya chuo Kikuu .
Mkurugenzi wa TASAF Makao makuu Bw. John Steven amesema, TASAF imeweza kufanikisha miradi mingi ndani ya Mkoa wa Morogoro yenye thamani ya sh. Bil. 66, kati ya hizo zimetolewa kwa njia ya mtandao wa simu na kupitia benki, huku akiekeleza uwepo wa ajira za muda zikizotolewa ambapo zimetumia kiasi cha Tsh. Bil. 23 na kutekeleza miradi 1500 Mkoani humo .
Bw. John amebainisha mafanikio mengine makubwa yaliyofanyika Mkoani humo kuwa ni pamoja na kuwafikia walengwa 43000 kati yao 21000 wamehitimu katika mpango wa TASAF na kuunda vikundi zaidi ya 3000 vikiwa na wanachama zaidi ya 36000 katika hivyo vikundi vimeweza kupatiwa kiasi cha Ths. Mil. 522 kwa ajili ya utekelezaji.