Top Stories

Yusuf Manji katoka Polisi, amekabidhiwa tena Mahakamani

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkabidhi mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kumaliza kumuhoji katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa kama Mahakama ilivyoamuru warudishwe baada ya Polisi kumaliza kuwahoji.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea na utaratibu kama ilivyo awali, ambapo ameahirisha hadi September 8, 2017.

Awali Mahakama hiyo iliruhusu Yusuf Manji na wenzake watatu kwenda kuhojiwa na Polisi kwa lengo la kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi wanayokabiliwa nayo.

Mbali na Yusuf Manji, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.

Unaweza kubonyeza play hapa chini kuitazama hii video

ULIPITWA? Yusuf Manji afikishwa Mahakamani ghafla…tazama kwenye hii video!! 

Soma na hizi

Tupia Comments