Top Stories

Maazimio matatu yaliyofikiwa na Chama cha Wabunge wanawake (+picha)

on

October 28, 2019 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameongoza Kamati ya Maazimio ya Semina ya Wajumbe wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika uliofanyika Mkoani Arusha.

Katika Semina hiyo iliyofunguliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Oktoba 27, 2019 imepitisha maazimio mbalimbali yakiwemo:-

1. Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika yatunge na kuhakikisha zinatelekezwa sheria zitakazohakikisha vyama vya siasa vinazingatia usawa katika nafasi za uongozi, sheria zitakazozuia ama kuadhibu makosa yanayohusiana na ukatili na unyanyasaji wa wanawake kipindi chote cha uchaguzi.

2. Serikali za nchi husika zihakikishe kunakuwa na mtaala wa elimu kuhusu jinsia.

3. Serikali husika na wadau wengine kuhakikisha inatolewa elimu juu ya masuala ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.

MBUNGE BILIONEA ANAEJISFU KUGAWA HELA JIMBONI, WANANCHI WAKE WANAMUITA BABA

Soma na hizi

Tupia Comments