Indonesia imetangaza rasmi kuhamisha mji wake Mkuu kutoka Jakarta kwenda Nusantara, Mashariki mwa Kisiwa cha Borneo.
Hofu juu ya uendelevu wa kiuchumi na kimazingira wa Jiji la Jakarta ambalo lina msongamano mkubwa ni moja ya sababu zilizopelekea uhamisho huo.
Kwa mujibu wa jukwaa la uchumi duniani (World Economic Forum) Jakarta ndio jji linalozama kwa kasi kupita Majiji mengine duniani .
Jiji hilo liko juu ya ardhi chepechepe, karibu na bahari na lenye kukabiliwa na mafuriko.
Mambo kadhaa yalizingatiwa kabla ya Nusantara kuchaguliwa kuwa Mji Mkuu zikiwemo faida za kikanda, ustawi na maono ya kitovu kipya cha uchumi.