Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 19, 2019 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo;
- Rais Magufuli amemteua Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kabunduguru alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu.
Kabunduguru anachukua nafasi ya Bw. Hussein Katanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
- Rais Magufuli amemteua Godfrey Gerald Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Elimu). Kabla ya uteuzi huo Mweli alikuwa Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Sheria na Katiba.
- Rais Magufuli amemteua Hashim Abdallah Komba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya uteuzi huo Bw. Komba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa.
Komba anachukua nafasi ya Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
- Rais Magufuli amemteua Hassan Abbas Rungwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
Rungwa anachukua nafasi ya Bakari Mohammed Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.
“MMECHAPWA NA RC NA MMERUDI HATUTAKI TUKUKUTE NA KOSA LOLOTE, TUTAKUFUZA” DC