Michezo

“Mnapofika hatua hii ni dalili kuwa hamjui Mnachokitaka”-Ridhiwani Kikwete

on

Siku kadhaa zilizopita Baraza la Michezo la Taifa BMT, liliagiza shirikisho la mpira Tanzania TFF kuhakikisha Yanga SC wanafanya mkuu tano mkuu na uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya wa club hiyo baada ya Mwenyekiti na makamu wake kujiondoa.

Mashabiki na wanachama wengi wa Yanga hawapendi Yussuf Manji aliyekuwa mwenyekiti wao aondoke katika klabu hiyo, hivyo walikuwa wanapinga suala la kujiuzulu kwa Manji na maagizo ya TFF kufanya uchaguzi Mkuu.

Mbunge wa Chalinze na shabiki mkubwa wa Yanga Ridhiwani Kikwete alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika maneno mazito yenye lengo la kuihamasisha Yanga kutii agizo la TFF na BMT kufanya uchaguzi na kama wanamtaka Manji wanayo nafasi ya kumchukulia fomu.

“Mnapofika hatua kama hii ni Dalili kuwa Hamjui Mnachokitaka. Uchaguzi ni Utaratibu wa Kawaida. Mnayemtaka mnaweza kwenda mchukulia fomu. Hakuna Busara ya kushindana Ubavu na Wasimamizi wa Mpira TFF”>>>Ridhiwani Kikwete

“Twendeni tukafanye Uchaguzi. Tunasimamisha Maendeleo ya Timu yetu kwa Ushabiki Usio na Macho ya Kujua Kesho yetu ikoje. Mwisho tutakuja tafuta Mchawi,Wakati Wachawi ni Sisi Wenyewe. Tusiwape Kichwa wakatamba” >>>Ridhiwani Kikwete

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments