Mix

Paul Makonda katangaza donge la Mil moja , majambazi wahusishwa ndani..

on

Leo March 18 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo, lakini kubwa ni hili la kutangaza kutoa zawadi ya milioni moja kila baad ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.

Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa, lakini nimeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha ;-Paul Makonda

Kuna watu wengi wana silaha halali na wawengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao, tunataka kujihakikishia tunzao silaha ngapi katika mkoa wetu kwamaana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu’ ;-Paul Makonda

Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha‘ ;-Paul Makonda

Ilikupita hii Video ya Agizo la kwanza alilolitoa Paul Makonda kama mkuu wa mkoa?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments