Mix

Watumishi hewa wamesababisha RC Makonda kufanya maamuzi haya leo…

on

Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amewaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote wa manispaa hiyo ili kusaidia kubaini watumishi hewa.

Makonda kafikia hatua hiyo baada ya watumishi hao kuwa wanampa idadi tofauti kila anapohitaji kupata taarifa, akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam Makonda anasema..

>>> ‘Mara ya kwanza mliniambia  tuna watumishi hewa  71, mara ya pili mkasema 87 na mara ya tatu wakapungua hadi 66 tena mara zote hizi ni idadi ya watumishi hewa kimkoa jambo ambalo roho wa Mungu alinikataza  kutangaza

Sasa Mungu kanipa njia ambayo nimewaambia wiki iliyopita, Leo hii wameongezeka wamefika watumishi hewa 209 huku ziai ya bilioni 2 zikipotea. Je, nisinge msikiliza Mungu si mgenifanya nikafukuzwa kazi?

Baada ya maelezo hayo Mkuu wa mkoa akawapatia mikataba ya viapo katika kutafuta watumishi hewa, lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe. 

IMG-20160502-WA0112

Watumishi wakila viapo mbele ya Mkuu wa mkoa

IMG-20160502-WA0111

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

USIKUTWE UMETUPA TAKA DAR, MAKONDA HACHEKI… KUNA VIJANA WAMEPEWA KAZI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments