Kubadilisha matumizi ya vitu siyo jambo la ajabu hasa kulingana na hitaji la wakati na mahali na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, biashara na utalii ambapo dunia imeshuhudia matumizi ya vitu vingi yakibalika.
Leo nimekutana na stori hii ya mjengo mmoja uliopo katika mji mkongwe wa Mikindani, Mkoani Mtwara, Tanzania ambao umebadilishwa matumizi yake mara kadhaa tangu kujengwa 1895 kutoka Ngome ya Ujerumani hadi Hotel ya Kitalii.
Nimekuwekea picha za muonekano wa nje na ndani wa hoteli hiyo, nakukaribisha uzitazame hapa chini ambapo mbali na kubadilisha matumizi na kuwa Hotel ya Kitalii, vyumba vyake vimepewa majina ya viongozi na watu maarufu akiwepo Mwalimu Nyerere, Dr. Livingstone na Chief Mkwawa, unaambiwa vitanda vya asili ndio vinavyotumika kwenye vyumba hivyo.
FULL VIDEO: Ulikosa kuyaona maamuzi ya Waziri Nape baada ya taarifa ya kuvamiwa Clouds TV? Bonyeza play kutazama hapa chini.
BAKING NEWSRE zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo