Habari za Mastaa

Mkali wa Amapiano kutumbuiza Kidimbwi Beach Dar , ifahamu ngoma aliyoimba na Mtanzania

on

Ikiwa bado Afrika Kusini wanaendelea kuchukua vichwa vya habari hususani kupitia muziki wao unaopeta kwasasa kwenye chart mbalimbali.

Sasa taarifa ninayotaka kukupatia ni kwamba Mkali kutokea nchini humo aitwae Musa Keys anatarajiwa kutumbuiza pembeni mwa fukwe za bahari maarufu kama Kidimbwi Beach iliyopo Mbezi  Dar es Salaam.

Miongoni mwa ngoma alizowahi kusikika ni hii akiwa na mtanzania Loui iitwayo Selema.

Selema ni kati ya ngoma pendwa inayofanya vizuri  hususani kupitia platform mbalimbali ikiwemo Spotify na nyinginezo.

Hata siku za hivi karibuni Msanii Loui alipofanya mkutano na Waandishi wa Habari alikiri na kutoa shukrani kwa Musa Keys kwani kupitia ngoma ya Selema mafanikio yameanza kuonekana hususani nchini Afrika Kusini.

Musa Keys anatarajiwa kutumbuiza siku ya Jumapili Mei 22, 2022 katika fukwe za bahari Dar es Salaam maarufu kama Kidimbwi Beach.

 

 

Tupia Comments