Page ya Instagram ya Label ya Konde Gang imetoa taarifa inayoeleza kuhusu kumalizika kwa mkataba kati ya Konde Music World wide na Msanii Country Wizzy.
Taarifa hiyo imeeleza ———> “Mkataba Kati Ya Konde Music Worldwide na Country Wizzy umemalizika hii leo tarehe 8 January 2022, kuanzia leo Country Wizzy atakuwa Msanii anaejitegemea baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili”.
“Konde Music Worldwide inamtakia kila lenye kheri Country Wizzy kwenye career yake ya music pamoja na maisha kwa ujumla 🙏, all the best Wizzy” ——— Konde Gang.