Habari za Mastaa

Mkataba wa Kobe Bryant na Nike wafika mwisho

on

Mke wa marehemu Kobe Bryant, VanessaBryant amechagua kutoendeleza mkataba kati ya marehemu mume wake na kampuni ya viatu ya Nike.

Imeelezwa, mkataba uliokuwepo ulifika kikomo tarehe 13 mwezi huu na yeye kama msimamizi wa mali ya marehemu alikataa kutia saini mkataba mpya wa kutengeneza viatu kwa jina la marehemu.

Vanessa anasema Kobe na Nike wametengeneza viatu vizuri kwa wachezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu ambavyo huvaliwa na hata mashabiki wasio wachezaji ulimwenguni kote.

Ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba, familia ya Kobe Bryant haikufurahia jinsi Kampuni ya Nike ilipunguza upatikanaji wa viatu vyake hasa baada yake kustaafu na baadaye kuaga dunia.

Kabla ya kifo cha Bryant taarifa ziliashiria kwamba mauzo ya bidhaa zake yalikua yanadidimia huku wengi wakilaumu Nike kwa kukosa kumpa mkataba wa maisha kama wa Michael Jordan na wa LeBron James.

Kwa sasa haijulikani jinsi familia ya marehemu Kobe Bryant itaendeleza urithi wake katika mchezo wa ‘Basketball’.

DC SABAYA AKUTA MAFUTA LITA TANO YANAUZWA ELFU 34, AKASIRIKA AMBANA MFANYABIASHARA “TUTAZINGUANA”

Soma na hizi

Tupia Comments