Dar es Salaam kwa sasa ni moja kati ya Miji mikubwa ambayo mandhari yake imekuwa ikibadilika kila uchao.
Julai 23, 2018 Rais Dkt. John Magufuli alizindua ujenzi wa daraja jipya la Salenda, ambalo litakuwa ni ukurasa mpya wa kutengeneza mandhari ya jiji la Dar es salaam.
Daraja hilo litajengwa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu, likiwa na urefu wa Kilomita 6.23 huku Kilomita 1.4 zikipita juu ya Bahari.
Daraja hilo litalopambwa na nguzo za Zege mithili ya Viganja vya Mikono ya Binadamu litaunganisha barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach katika makutano ya barabara za Kenyatta na Toure ambapo unatekelezwa kwa Sh.Bil 556.1 huku serikali ya Tanzania ikitoa Bil.49.457.