Mke wa Joaquin “El Chapo” Guzman anatazamiwa kuachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani kwake huko California siku ya Jumatano, baada ya kuhukumiwa kwa kusaidia kuendesha genge la kuuza dawa za kulevya la Mexico ambalo mumewe alikuwa mkuu wake, kulingana na rekodi za gereza.
Emma Coronel Aispuro alihukumiwa mwezi Novemba 2021 hadi miezi 36 katika jela ya shirikisho baada ya kukiri kosa la kutakatisha fedha na kula njama ya kusambaza kokeini, meth, heroin na bangi kwa ajili ya kuingizwa Marekani. Pia aliamriwa kulipa faini ya karibu $1.5 milioni.
Aispuro alihamishwa kutoka gereza la shirikisho huko Texas, hadi nyumbani huko Long Beach, California, mnamo Juni, kabla ya kuachiliwa kwake.
Ni kawaida kwa wafungwa ambao wameonyesha tabia njema katika gereza la shirikisho kuhamishwa hadi nusu ya nyumba hadi miezi sita kabla ya kuachiliwa kwao, kulingana na afisa wa Ofisi ya Magereza.
Alikamatwa Februari 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles, nje kidogo ya mji mkuu wa taifa hilo, na kukutwa na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya na mashtaka ya utakatishaji fedha na mahakama ya Washington, D.C. baadaye mwaka huo.
Katika hukumu yake, Aispuro, kupitia kwa mkalimani aliomba msamaha, na kuapa kuwa atawafundisha binti zake mema na mabaya.