Karibu mwezi mmoja baada ya mapinduzi ambayo yaling’oa mamlakani rais be zamani Ali Bongo, mkewe, Sylvia Bongo, ameshtakiwa kwa ‘utakatishaji wa fedha haramu, wizi na kughushi nyaraka mbalimbali’.
Kulingana na redio ya Kifaransa inasema kuwa kulingana na mwendesha mashtaka André Patrick Roponat, Sylvia Bongo alisikilizwa mnamo Septemba 28, 2023 na jaji anayechunguza tuhuma zinazomkabili. Hapa sasa anashtakiwa kwa “utakatisha wa fedha haramu, wizi, na kughushi nyaraka mbalimbali” na amewekwa nchini ya kifungo cha nyumbani.
Hali yake imefafanuliwa, tangu mapinduzi ya Agosti 30, Sylvia Bongo, mwenye uraia pacha (Gabon na Ufaransa) anawekwa mahali pasipojulikana, bila kujua hatima yake. Mawakili wake pia waliwamewasilisha malalamiko nchini Ufaransa kwa mteja wao kuwekwa kizuizini kiholela na wanalaanikuendelea kushikwa mateka.
Waangalizi wengi wanashuku Sylvia Bongo kuwa katikati mwa mfumo mkubwa wa ufisadi kwenye ngazi ya juu serikalini.
Mara tu baada ya mapinduzi, msaidizi wake Kim Oun alikamatwa nyumbani kwake. mabegi yaliyojazwa pesa yalikamatwa ofisini kwake na szehemu zingine.
Mtu huyo alisema kuwa fedha hizo ni za Sylvia Bongo, na kwamba ofisi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na yeye moja kwa moja.