Top Stories

Mke wa Rais wa Haiti, afunguka alivyoshuhudia kifo cha mumewe “Risasi zilitawala”

on

Kwa mara ya kwanza tangu aliyekua Rais wa Haiti Jovenel Moïse kuuwawa nyumbani kwake mbele ya Mke wake July 7,2021. Mke wake huyo aitwae Martine Moise ambaye alisafirishwa kwenda Marekani kwa ajili ya matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye shambulio hilo, amezungumza kwa mara ya kwanza.

First Lady huyu amesema kuwa mashambulizi siku hiyo yalianza usiku wa saa saba ndipo walianza sikia risasi zinapigwa kwenye chumba chao na wakaamua kujificha lakini Watu hao hawakuishia hapo kwani waliingia mpaka ndani ya nyumba na kuvunja mlango na kuingia mpaka chumbani kwao.

Anasema wale Wauaji walikuwa wametumwa kwani walivyovunja chumba chao walikuwa na kazi moja tu ya kutafuta nyaraka na walipozipata wakapiga simu na kuwaambia waliowatuma kuwa wameshazipata na kisha kumsogelea Rais na kupokea maelekezo ambayo yaliashiria kuwa ndie Mtu sahihi anaetakiwa kuuwawa.

Mpaka wakati huo tayari Rais na Mke wake walikua wameshajeruhiwa kwa risasi nyingi na Wauaji hao wakapewa agizo kuwa wamalizie kumuua Rais Jovenel Moise “hatukujua kama wangefanikiwa kufika kwenye chumba tulikojificha maana nje tulikua na Walinzi 30 au 50″- Martine Moise

Ayo TV imekuandalia stori kamili hapa bonyeza play kufahamu mwanzo mwisho.

GUMZO!! MUOSHA MAGARI ALIENDA KUTAMBA NA GARI LA MTEJA APATA NALO AJALI DODOMA

 

 

Tupia Comments