Mpiga picha wa Kenya Jacktone Odhiambo amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela kwa kumuua mwenzake wa nyumbani, mwanaharakati wa LGBTQ+ Edwin Kiprotich Kipruto, maarufu kama Edwin Chiloba, karibu miaka miwili iliyopita.
Jaji Reuben Nyakundi alisema hukumu hiyo ya miongo mingi ilitokana na “namna ya kishetani” ya mauaji hayo.
Chiloba, mwanamitindo mwenye umri wa miaka 25, alizidiwa hadi kufa na mwili wake kutupwa kwenye sanduku la chuma kando ya barabara mjini Eldoret.
Mauaji hayo yalileta mshtuko katika jumuiya ya LGBTQ+ nchini Kenya.
Jaji Nyakundi alisema Odhiambo, 25, hakuonyesha kujutia mauaji hayo.
Hata hivyo, baada ya kusomewa hukumu hiyo, Odhiambo alizua tafrani katika mahakama hiyo kwa kuanguka chini na kulia.
“Nimezingatia mambo yote na kugundua kuwa Odhiambo alikuwa mtu wa kulipiza kisasi aliyetekeleza mauaji ya rafiki yake wa karibu,” akasema hakimu.
Chiloba na Odhiambo walikuwa wahudumu wa nyumbani wakiishi karibu na Chuo Kikuu cha Eldoret ambapo Chiloba alikuwa mwanafunzi. Kulikuwa na baadhi ya ripoti kuwa wanaume hao wawili walikuwa kwenye uhusiano.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mark Mugun, uliambia mahakama kuwa Odhiambo alitapanya pesa za mwanaharakati huyo baada ya kumuua.
Ushahidi kutoka kwa mashahidi 23, vikiwemo vipimo vya DNA vilivyomhusisha Odhiambo na eneo la uhalifu, pia uliwasilishwa na upande wa mashtaka.
Mwili wa Chiloba ulikutwa ukiwa na soksi mdomoni na kipande cha nguo amefungwa usoni.
Uchunguzi wa maiti ulionyesha kuwa alikuwa amekufa kutokana na kukosa hewa ya kutosha, iliyosababishwa na kuvuta pumzi.
Ushahidi huo pia ulionyesha mshukiwa alimdhalilisha Chiloba kabla ya kujitoa uhai.