Michezo

USAJILI WA YONDANI: Manara asema “Mimi ndio msemaji wa SIMBA SC”

on

Moja kati ya stories zinazochukua headlines kwa sasa katika soka la bongo ni ishu ya usajili wa wachezaji kutoka club moja kwenda nyingine, imekuwa kawaida duniani kote mchezaji fulani kuhusishwa kwenda club fulani.

Haji Manara

Kwa sasa kwa Tanzania moja kati ya wachezaji wanaohusishwa kuhama vilabu vyao ni beki wa Yanga aliyemaliza mkataba wake Kelvin Yondani ambaye anahusishwa kwenda Simba SC, baada ya tetesi kuwa nyingi afisa habari wa Simba Haji Manara ameandika maneno haya kupitia ukurasa wake wa instagram kwa wanaomuuliza kuhusiana na ishu hiyo.

“Shida yangu mimi ni moja tu…jambo linazushwa halafu napigiwa eti nithibitishe!! Kawaulizeni waliotoa taarifa hii..Simba haipo na mimi ndio spokesman wa klabu”>>> Haji Manara

Kelvin Yondani

Cristiano Ronaldo alivyowasili Turin na private jet

Soma na hizi

Tupia Comments