Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (CCM) Rajabu Abdallah, ametoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani kuhakikisha wanarekebisha mabati ya moja ya majengo ya hospitali hiyo ambayo hayana viwango stahiki. Maagizo hayo yalitolewa wakati wa ziara yake hospitalini hapo, ambapo alishuhudia hali ya uchakavu wa mabati na majengo huku Serikali tayari ilishatoa kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali hiyo.
Aidha, katika ziara hiyo, MCC Rajabu alikabidhi vifaa vya kisasa vya mpakato aina ya iPad nane, kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni 5. Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa uongozi wa hospitali kwa lengo la kuboresha mfumo wa kidijitali wa utoaji huduma kwa wagonjwa. hatua hiyo inalenga kuimarisha huduma za afya kwa teknolojia ya kisasa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Gift Msuya, katika kushughulikia maagizo aliyoyapokea, huku akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa (MCC) Rajabu kwa msaada wa vitendea kazi katika hospitali ya Pangani.
“Hii ni hatua nzuri inayolenga kuboresha huduma za afya na maendeleo ya wilaya hii”.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Japheti Semeo amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Mhe. Rajabu Abdallah, kwa msaada wa vitendea kazi vya kisasa vilivyotolewa kwa hospitali ya Wilaya ya Pangani. Alisema kuwa vifaa hivyo, hususan iPad za kisasa, vitasaidia kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na kuharakisha utoaji wa huduma bora.
Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa Japheti Semeo aliahidi kuwa hospitali hiyo itatumia vifaa hivyo kwa manufaa ya wananchi, huku akisisitiza kuwa “teknolojia hii ya kisasa itapunguza changamoto nyingi zilizokuwepo katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya,Pia kuhusu ukarabati wa mabati na miundombinu mingine, kama alivyoagiza MCC Rajabu, ni muhimu sana kwa kuboresha mazingira ya kazi na huduma kwa wagonjwa”
Katika kumalizia, aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa weledi na kutumia rasilimali zilizopo kwa uangalifu ili kufanikisha azma ya serikali ya kuimarisha sekta ya afya nchini.