Michezo

Mkude arejea Simba

on

Staa wa Soka na Mchezaji Mwandamizi wa Simba SC Jonas Mkude leo ameripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2021/2022 baada ya kuwa nje ya Timu kwa zaidi ya miezi miwili kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

June 07, 2021 Kamati ya Nidhamu ya Simba SC chini ya Mwenyekiti wake Selemani Kova iliahirisha hukumu ya tuhuma za utovu wa nidhamu kwa kiungo Jonas Mkude na kuagiza kuwa Mkude akapimwe ili kujua kwa nini ana makosa ya kujirudia.

Simba SC sasa inaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na Wachezaji wamewasili leo kama Kocha wao Mkuu Didier Gomes alivyoagiza, inasemekana Simba SC itaweka kambi ya maandalizi nchini Morocco.

MESSI ASHINDWA JIZUIA AMWAGA MACHOZI MBELE YA WACHEZAJI WENZIE

Soma na hizi

Tupia Comments