Top Stories

Mkurugenzi aanguka ghafla akihojiwa na Waziri Jafo (+video)

on

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo Dodoma leo ikiwemo barabara ya Swaswa kwa kiwango cha lami ya KM 1.8, eneo la kuegesha Malori ya mizigo Nala pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa Sekondari ya Itega na Lukundo, zote za Dodoma.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Swaswa ametoa siku 26 kwa Mkandarasi wa mradi huo ambaye ni Kampuni ya SKOL, kukamilisha kazi vinginevyo anapaswa kutopewa tena kazi Tanzania.

Sasa katika hali ambayo haikutarajiwa wakati akitoa maelezo hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya hiyo ya SKOL, Vicent Massawe alionesha kuishiwa nguvu na kudondoka chini.

NDANI YA MAHAKAMA WAMETAZAMA VIDEO YA ZITTO KABWE MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments