Ni June 8, 2023 ambapo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA, Plasduce Mbossa amefanya mahojiano katika kituo cha Clouds Media Group kuelezea sakata linaloendelea mitandaoni juu ya Bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini, TPA, Bw. Plasduce Mbossa akielezea kuwa licha ya kuwepo kwa Mkataba huo unaelekeza kwamba kqma tukitaka kushirikiane lazima tukubaliane na hiyo mikataba mingine.
“Kwenye mkataba hakuna sehemu kuna miaka 100, nafikiri walioleta hilo wana sababu zao na ni upotoshaji wa hali ya juu. Mkataba uliopo una kifungu kinachosema kwamba kuna muda wa miezi 12 wa kuridhia na ikipita miezi 12 bila kuridhia maana yake mkataba utakuwa umekwisha”-Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
“Pia kama tutaingia kwenye negotiation na tukashindwa kufikia muafaka na kusaini mikataba ya utekelezaji maana yake mkataba utakuwa umekwisha.” – Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
“Miaka yote tumekuwa tukifanya wenyewe, tunachotaka ni kupata manufaa tunavyoweza kuyapata kutoka kwao. Lakini pia mkataba huu unasema ni kuwajengea uwezo Watanzania”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
“Sasa hivi tuna Kampuni kubwa za Watanzania. Kipindi cha nyuma Kampuni nyingi za usafishaji zilikuwa zikitoka Kusini mwa Afrika ndio zilikuwa zikifanywa kazi hapa lakini sasa hivi tuna Kampuni kubwa kabisa za Kitanzania na wafanyabiashara wakubwa. Na Kampuni hii ya DP WORLD ana vitu ambavyo tunadhani tukishirikiana naye vitatusaidia sisi kupiga hatua kutoka hapa tulipo”- Plasduce Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)