Ni Machi 25, 2023 ambapo nakukutanisha na Ahmed Asas ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Maziwa Tanzania, ‘Asas Dairies Ltd’ na kuzungumza nae yale tusiyoyajua kuhusu Uzalishaji wa Maziwa.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV alizungumza kuhusu idadi ya wafugaji waliopo katika mikoa mitatu ikiwemo Mbeya, Njombe na Iringa pamoja na mengineyo.
“Tunawafugaji Elfu 6500, kwa mikoa mitatu Mbeya Njombe na Iringa lakini kwa mwaka mmoja tunarajia kuongeza Wafugaji Elfu 10000, na kwa siku kwa upande wa Mkoa wa Mbeya tunauwezo wa kuzalisha Lita Elfu 20 kwa siku ambapo tunafuata na Malori maalum”
“Hapo Mwanzo kampuni ilikuwa ina zalisha Elfu moja kwa siku lakini kwasasa Kiwanda ina uwezo wa kuzalisha lita Laki moja na nusu huku uzalishaji halisi ukiwa chini ya lita Elfu Hamisi kwa siku”- Ahmed Asas
“Kwasasa Kampuni ya Asas inapata maziwa kutoka mashamba yake binafsi wafugaji wakati na wakubwa na wafugaji moja moja na wafugaji wadogo walio kwenye vikundi na vyama vya ushirika”- Ahmed Asas
“Licha Changamoto mbalimbali ambazo kampuni hii imepitia bado naamini ili kukua zaidi tunahitaji kuwainua wafugaji wadogo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa Maziwa, hivyo tunawekeza rasirimali nyingi katika kuwanuia wafugaji wadogo wapatao Elfu 6500”- Ahmed Asas
“Lisha ya Makao makuu yake kuwepo mkoani Iringa Kampuni ya Asas ilienda zaidi ya Kilometa Mia nne kutoka Mkoani Iringa ili kuwafikia wafugaji mbalimbali ili kufanya biashara kwa pamoja, Kampuni ya Asas kwa kushirikiana na wafugaji tumetumia mfumo wa kuunda vikundi ili kuwafikia wafungaji wengi wenye uhitaji ambapo jumla ya vikundi vilivyopo kwasasa ni jumla ya 140”- Ahmed Asas
“Kwa Wilaya kama ya Rungwe na Isanu Busokelo ambapo ndipo kuna Uzalishaji mkubwa wa Maziwa, kampuni ya Asas japo tulikutana na changamoto ya Barabara ila tuliweza kuwafika na hatimae leo hii wananufaika na kampuni yetu- Ahmed Asas