Ni Mei 14, 2022 ambapo muda huu benki ya CRDB inafanya Semina maalumu ya kutoa Elimu kwa Watanzania namna ya kuwekeza katika sekta Mbalimbali.
Akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi wa CRDB Abdulmajid Mussa Nsekela awataka Watanzania kuwekeza katika Sekta Mbalimbali ili nchi inufaike kiuchumi.
‘Uwekezaji ni jambo la muhimu sana maendeleo yote ya Uchumi tunayosema sasa yanatokana na uwekezaji, Uchumi unakuwa pale panapokuwa na wawekezaji wengi unapowekeza ajira zinakuwa nyingi Walipa kodi wanakuwa wengi kwahiyo Serikali inakuwa inapata wa mapato mengi’- Nsekela
‘Wote tunafahamu Serikali yetu ya Awamu ya Sita inafanya jitihadi ya kuleta wawekezaji kutoka nchi mbalimbali tumshukuru Muheshimiwa Rais kwa kulifanya jambo hili ili nchi yetu isonge mbele’- Nsekela
‘Benki yetu ya CRDB ni Benki kinara kwa maana ni Benki yenye ubunifu mkubwa huduma yetu ya kwanza kutoa ushauri mteja anaweza vipi kuwekeza, ama kuwapa solution kwa ambao wanafungua viwanda lakini vilevile tumekuwa tukitoa masomo juu ya elimu ya Soko la Hisa‘- Nsekela
‘Ushirikishwaji wa wadau katika CRDB Uwekezaji Day mwaka huu umeboreshwa sana, maboresho haya yametokana na kauli mbiu yetu, tumekuwa tukisafiri sana na tumekuwa tukipata mawazo mengi watanzania wengi wanahitaji kufahamu namna ya kuwekeza kwani ni mafunzo ambayo naamini yataleta chachu ila kuwasaidia watanzania namna ya kuweza kuwekeza katika kile wanachokiamini’- Nsekela
‘Kuna Kilimo, Viwanda, Teknolojia haya yote hayatawezekana kama watanzania hawatapata somo ndio Maana CRDB inafanya Semina hii ili kuwafungua Watanzania wenye uhitaji wa kuwekeza katika maeneo tofauti tofauti hususani sekta nilizozitaja’- Nsekela
Aidha Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Uwekezaji TIC, John Mathew Mnali akazungumza kuhusu wale wenye uhitaji wa kuwekeza katika Sekta ya Mafuta.
‘Kwa Tanzania Shughuli za uwekezaji zinaratibiwa na taasisi kadhaa ingawa majukumu ya kunada fursa zote za uwekezaji zilizopo nchini na kwa wale wenye uhitaji wa kuwekeza katika Sekta ya Madini hawa tunawashauri waende katika wizara ya Madini ambapo Kamishna anatoa leseni kwa wachimbaji wadogo, Wchimbaji wakati, wachimbaji Wakubwa’– John Mathew
‘Lakini pia kuna Wawekezaji wengine ambao labda wanataka kushirikiana na wawekezaji wa nje kama Petrol ama masuala ya utafiti tunawashauri kuwasiliana wakawasiliana na Wizara ya Nishati ili waweze kupata Elimu kupata muongozo sahihi’- John Mathew
‘Kwa wale ambapo wanahitaji kuwekeza visiwani Zanzibar kule kuna taasisi inaitwa ZIPA ambayo itakupa Elimu ya kutosha na muongozo maeneo yanayoruhusiwa kuwekeza kile ulichonacho’- John Mathew
Hayo ni baadhi ya kile kinachojiri katika Semina Maalum iliyoandaliwa na CRDB Bank kuhusu Uwekezaji.