Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura ametolea ufafanuzi wa shauri la kimkataba baina na Mchezaji Feisal Salum na Klabu ya Yanga muda mchache baada ya mchezaji huyo kufika kwenye Ofisi za TFF kwa ajili ya kusikiliza shauri lake.
Wambura amesema kuwa bado majadiliano yanaendelea baina ya pande zote mbili hivyo Kamati ya TFF itakuja kutolea majibu juu ya kesi hiyo.