Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika, Dkt Faustine Ndugulile, ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, amewaasa wananchi kujenga utaratibu wa kupima afya zao ili kuweza kuja hali zao za kiafya
Dr Ndugulile amesema hayo wakati akizindua kambi ya siku tatu ya matibabu ya macho iliyofanyika katika hospitali ya vijibweni Wilayani Kigamboni
Kambi hiyo matibabu ya siku tatu kuanzia Oktoba 5-7,2024 imeandaliwa na Klabu ya Lions Club DSM (Host) pamoja na Taasisi ya LALJI FOUNDATION za Jijini Dar es Salaam.
‘Sasa hivi katika afya ni muhimu kujua hali yako ya kiafya, ni muhimu sana taarifa muhimu kuhusu afya yako ikiwemo uzito wako,urefu wako,presha yako ni kiasi gani,kujua kiwango chako cha sukari kwa sababu Ukijua hali yako ya kiafya itakusaidia kujua namna ya kutunza afya yako na kutokujua hali yako ya kiafya ni hatari sana kwa afya yako,” amesema Dr Ndugulile
Akizungumzia umuhimu wa kambi hiyo Rais wa klabu ya Lions Club DSM (Host), Bwana Mahmood Rajvani amesema kuwa lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwezesha matibabu ya macho ambayo mara nyingi yana gharama kubwa hususan kwa wananchi wa kipato cha chini
“Kila mwaka tumekuwa tukifanya kambi hizi za matibabu ya macho, lengo letu ni kumuunga mkono Rais wetu Dkt Samia Hassan katika kuwahudumia wananchi wote nchini Tanzania hasa wenye vipato vya chini” Alisema Mahmood Rajvani
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya LALJI FOUNDATION, Bwana Imtiaz Lalji ameeleza kuwa kambi hiyo ya matibabu ianatarajia kuhudumia wagonjwa takribani 3000.
“Tunategemea mpaka mwisho wa kambi hii tutakuwa tumehudumia walau wagonjwa 3000 kutoka sehemu mbalimbali za Kigamboni na pamoja na wananchi kutika wilaya za jirani” Imtiaz Lalji
Mrisho Bindo ambaye ni mkazi wa kigamboni na mnufaika wa kambi hiyo ya matibabu ameshukuru waandaaji wa kambi hiyo akileza kuwa imewasidia kupima afya zao huku akitoa rai kwa taasisi nyingine kufanya camp kama hizo za matibabu.