Mkurugenzi wa Masoko, Wanachama na Mashabiki wa Yanga SC Ibrahim Samuel yuko nchini Botswana katika Jiji la Gaborone kwa ajili ya kutoa Elimu ya mfumo wa mabadiliko na uendeshaji wa klabu wenye kuleta thamani kwa wanachama na Washirika wa kibiashara kwa vitendo.
Mkurugenzi huyo amekwenda nchini humo na kukutana na uongozi wa Klabu ya Township Rolles na kuwapa elimu hiyo ya mfumo wa kisasa jinsi ya kujiendesha.
“ Tunapata nafasi hii kutokana na vijana kuaminiwa na kufanya kazi nzuri. Rais wetu wa Yanga SC Hersi Said haiishii kuihudumia Yanga SC peke yake, anahudumia hadi timu nyingine ndiyo maana hadi mimi unaniona niko huku kwa ajili ya kutoa darasa kwa wenzetu Township Rolles ” alisema Ibrahim.
Mkurugenzi huyo licha ya kutoa elimu hiyo, lakini pia alitoa zawadi ya jezi ya Yanga SC kwa baadhi ya viongozi wa timu hiyo.
Yanga SC klabu ya kwanza Afrika kuanza kuvikomboa vilabu vingine na Elimu ya mabadiliko ya uendeshaji chini ya Rais wake Mhandisi Hersi Said na kamati yake Tendaji.