Ikiwa leo ni mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA unaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jiji Dar es salaam, AyoTV imejionea ulinzi mkali wa jeshi la Polisi ambapo askari wa kutuliza ghasia FFU wakiimalisha ulinzi.
AyoTV imeongea na kamamda wa Kanda maalum Dar es salaam SACP Jumanme Muliro ambaye amesema wameimalisha ulinzi kutokana na eneo la mlimani city ni sehemu ya biashara ambapo watu wengi hufika na uwepo wa bank nyingi lakini pia uwepo wa mkutano huo ambao unakusanya watu wengi hivyo swala la ulinzi ni lazima.
” kwenye watu wengi panaweza pia kuwepo kuwa na mambo mengi kwahiyo sisi jukumu letu mahali hapa pawe salama na kuimalika kama ilivyokuwa wakati wote nyuma, watu wametishiana katika mitandao X anasema hivi na Y anasema hivi,sisi ambao tumepewa jukumu la ulinzi hatuwezi kuacha pakawa na vurugu lazima tuimalishe ulinzi na watu wengi katika makundi haya mawili wamefurahi sisi kuwepo hapa wanajua wapo salama zaidi”