Mkuu wa jeshi la Israel alijiuzulu siku ya Jumanne, akichukua jukumu la “kushindwa” kwake kusitisha shambulio la Hamas la Oktoba 7, siku chache baada ya mapatano tete kuanza kutekelezwa kufuatia miezi 15 ya vita katika Ukanda wa Gaza.
Katika barua yake ya kujiuzulu Halevi amesema sababu kubwa iliyomfanya kujiuzulu kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuzuia uvamizi huo.
Hatahivyo, amesema anafarijika kuona jeshi la Israel limeweza kupata mafanikio makubwa wakati wa uongozi wake
Wakati huo huo kiongozi wa upinzani wa Israek Yair Lapid ameitaka serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ijiuzulu baada ya Halevi kujiuzulu.