Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi TanzaniaMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa kutekeleza vema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo alipozungumza na Jenerali Mabeyo ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya Jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria.
Rais Dkt. Mwinyi amemtakia kila la heri Mabeyo katika maisha yake ya kustaafu hasa ikikumbukwa amelitumikia kwa mrefu Jeshi hilo na kufanya mambo mengi yatakayoacha alama.
Kwa upande wake Jenerali Mabeyo amesema Jeshi la Ulinzi Tanzania litaendelea kumkumbuka Rais Dk. Mwinyi kwa busara na hekima zake katika kuzishughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo ambalo hatimae limepata mafanikio makubwa.
HAJI MANARA ATANGAZA KUMTAFUTA AHMED ALLY WA SIMBA “DOGO ANA MBINU ZAKE ZA KISASA”