Mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) amewataka waasi wa kundi la M23 kusitisha harakati zao na kuondoka nchini humo.
Jean-Pierre Lacroix amesema ni muhimu kwa kundi la waasi la M23 kusitisha shughuli zake na kuondoka katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema, kukiuka mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Kongo ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa na Hati ya Umoja wa Mataifa. Mkuu wa MONUSCO ameeleza haya katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la UN
Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa kikosi cha MONUSCO kutoka Afrika Kusini na mwingine kutoka Uruguay wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa mapiganoni huko Kongo.
Askari waliojeruhiwa wanaendelea kupatiwa matibabu katika mji wa Goma.
Jean-Pierre Lacroix amesema kuwa mashambulizi dhidi ya askari jeshi wa kulinda amani yanaweza kuhesabiwa kama uhalifu wa kivita.