Mkuu wa kitengo cha Usalama na intelijensia nchini Denmark DDIS Lars Findsen (57) anashikiliwa na Polisi juu ya tuhuma za kuvujisha habari na data za siri.
Findsen alifikishwa Mahakamani jana jijini Copenhagen lakini alikana tuhuma hizo. Mwanzoni mwa skendo hiyo walioshikiliwa walikuwa wanne wakiwemo wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa huduma za intelijensia za nchini humo. Kwa sasa Findsen ndio mtuhumiwa namba moja wa kesi hiyo.
Tetesi kuhusu kesi hiyo inayoendeshwa kwa usiri mkubwa zinasema kuwa pamoja na tuhuma nyingine idara hiyo iliipa idara ya Usalama ya Marekani uwezo wa kuona data nyingi zikiwemo za viongozi wa Ulaya pamoja na mazungumzo yao binafsi.
Iwapo atakutwa na makosa Findsen anaweza kufungwa jela kwa miaka 12.